Thursday 20 August 2015

magonjwa ya kuku na jinsi ya kuyadhibiti


habari za wakati huu wapendwa wafugaji na wasio wafugaji,wasomi wa machapisho yetu kwa ujumla.katika toleo hili tunachambua magonjwa mbalimbali ya kuku.magonjwa ya kuku husabibishwa na vitu mbali mbali ikiwemo virusi,minyoo,bakteria,uchafu,wadudu na hata upungufu wa virutubisho katika vyakula vya kuku hawa.magonjwa ambayo husababishwa na virusi hua ni vigumu sana kutibika hivyo mfugaji hushauliwa kuwapa chanjo ya magonjwa hayo.mfano ni mdondo(new castle disease).ugonjwa huu ni hatari sana kwa kua humaliza kuku wengi kwa wakati mmoja.wengine huita huu ugonjwa kideri.
   Mdondo(new castle disease).
kama binadamu aogopavyo ugonjwa wa UKIMWI,basi wafugaji wengi huogopa sana ugonjwa wa mdondo,pia huitwa kideli(newcastle disease).huu ni ugonjwa HATARI unaosababishwa na virusi pia ni ugonjwa huu hauna tiba.Hivyo mfugaji anatakiwa kuwapa chanjo mapema kabla ugonjwa haujafika eneo hilo.dalili za mdondo ni kama.
1.kuku kukohoa au kuhema kwa tabu
2.manyoya ya kuku huvurugika na kua katika hali isiyo ya kawaida.
3.kuku huarisha kinyesi cha kijani
3.kupoteza hamu ya kula na mabawa kupoza
4.kizunguzungu na kuanguka chali
5.kupoteza fahamu

ugonjwa huu hupelekea kuku wengi kufa kufikia hadi asilimia 50 hadi 100 kama usipo dhibitiwa mapema.
Namna ya ugonjwa unavyosambaa
1.virusi hawa huweza kusambaa kwa njia ya hewa au upepo husafirisha virusi hawa.
2.kinyesi cha kuku mwenye mdondo kikikanyagwa na mtu,baiskeli au wanyama wengine na kusafirishwa kwenye banda la kuku,ugonjwa huu huweza pia kusambaa.
3.kuku alie kufa kwa mdondo asipo zikwa vizuri au kuchomwa moto,kuku mzima akila mabaki hayo,kuku hao watakua katika hatari ya kupata mdondo.
JINSI YA KUPAMBANA NA MDONDO
Kama ilivyo elezwa hapo juu,gonjwa hili halina tiba.lakini kuku wakipewa chanjo kwa wakati hua katika usalama.kuna chanjo kama;
1.LASOTA
chanjo hii ni ya vidonge,kidonge kimoja huchanganjwa na maji safi.chanjo hii tolewa baada ya siku tatu kisha rudi baada ya wiki tatu  na rudia kila baada ya majuma manne au kutokana na uonavyo.kabla ya kuku kupewa dawa hii yapaswa wasipewe maji kwa masaa kadhaa kwa siku hio na muda wa kupewa maji basi wapewe sehemu yenye kivuli.
chanjo hii hupatikana katika maduka mbali mbali ya mifugo.
2.Chanjo ya Thermostable 1-2,dawa hii inahuwezo mkubwa wa kustahimili joto,watu wasio na majokofu basi tumia dawa hii ila hifadhi sehem kavu na isio na joto.dawa  hii huweza kukaa wiki mbili baada ya kufunguliwa kwa Mara ya kwanza.
EPUKA YAFUATAYO
kununua kuku katika minada na kuleta bandani
kuruhusu kila mtu kuingia katika banda la kuku
kuacha mabaki ya kuku walikufa ovyo katika mazingira ya kuku
pia,endapo kuku wengi walikufa katika banda hilo basi ni vyema usilete kuku wengine katika banda hilo angalau kwa ,mwezi au zaid.
Tenganisha kuku wenye dalili za ugonjwa na kuku wengine.
ZINGATIA USAFI WA BANDA NA VYOMBO VYA KUKU WAKO.

usikose kutembelea blog hii kwa taarifa nyingine zaidi kuhusu ufugaji wa kuku



0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Pages

//]]>