Wednesday, 2 September 2015

KUTOTORESHA VIFARANGA


Habari za wakati huu wafuatiliaje wa machapisho yetu.Leo tutatazamia njia kuu mbili za kutotoresha mayai ya kuku wa kienyeji,njia hizo ni kumuacha kuku kutotoa mwenyewe na kumuwekea mazingira.njia ya pili ni kwa kutumia mashine za kutotoreshea.


NJIA ASILIA
kwa kutumia njia hii kuku ataachwa kutaga,kuatamia,na kutotoa mwenywe.mfugaji aandae mabox au mfuko kisha aweke vitu vyenye kutunza joto kama mchanga au matambaa kisha mabox hayo yawekwe katika mabanda ya kuku sehemu tulivu na yenywe kivuli


kuku hugata mayai 10-14 kutegemeana na aina ya kuku.kuku huweza kutotoa mayai 8-14


NJIA YA KISASA
Baada ya kuandaa sehemu ya kuku kutagia,kusanya mayai kila siku na kuweka katika trei.Uwekaji wa mayai hayo,sehemu kubwa ya yai iwe juu na incha yake iangalie chini.Hii husaidia katika utotoleshaji kwenye mashine.mashine hutotoresha vizuri zaidi endapo mayai yatakua yalikusanywa katika kipindi kifupi kuanzia siku 1-6 na kuwekwa katika mashine (incubator)

 MASHINE YA KUTOTORESHEA VIFARANGA(INCUBATOR)
Hii ni mashine ambayo hufanya kazi ya kuatamia na kutotoa mayai.mashine ina uwezo wa kutoto mayai mengi,mashine ndogo huweza kutotoa mayai 25-50.mashine hii hutoa joto sawa na joto la tetea,inashauliwa kugeuza geuza mayai kwa siku angalau mara tatu katika mashine ili kupata mazao bora zaidi.


CHANGAMOTO YA MASHINE HII
Inahitaji utaalamu kuitumia
inahitaji muda mwingi kukaa nayo karibu
ni gharama kuiendesha.

Thursday, 27 August 2015

NJIA ASILIA ZA KUTIBU KUKU


ni matumaini yangu wote mu wazima wa afya.katika chapisho hili tutaangalia njia za asilia za kutibu kuku kwa kutumia shubiri mwitu na majani ya mpapai.

SHUBIRI MWITU NA JINSI YA KUIANDAA
Tafta majani kadhaa ya shubiri mwitu kisha chana chana vipande vidogo vidogo kisha changanya na pumba na kuvianika.Mchanganyiko huo uanikwe juani.Baada ya kukauka vizuri twanga mchanganyiko huo ma kisha chekecha kupata unga.

majani ya shubiri mwitu

matumizi.
kuku walipata vidonda kutokana na magonjwa mbali mbali ,safisha vidonda vya kuku vizuri kisha pakaa unga huo katika vidonda hivyo.

pia hutumika kama chanjo.
kata kata vipande vidogo vidogo vya majani ya shubiri mwitu kisha changanya na maji na kuku wapewe maji hayo kwa wiki angalau mara tatu.maji yabadilishwe mara kwa mara kabla hayajaharibika.

MPAPAI NA NAMNA YA KUANDAA
mpapai husaidia kuku wanao harisha.
mti wa mpapai


maaandalizi
twanga majani ya mpapai kisha changanya na maji.majani mawili na maji lita mbili au moja na nusu.kuku wapewe maji hayo kwa siku nne lakini maji hayo yatengenezwe kila siku yasiachwe kiporo ili kutumika siku nyingine.


Ikitumika kama chanjo fanya kama ifuatavyo.

andaa kisamvu cha mpapai kisha changanya na pumba kg 2 mwsho weka na maji katika mchanganyiko huo kisha wape kuku lakini chakula hiki kiwekwe kulingana na idadi ya kuku kwa kua kisipo malizika mapema hualibika kirahisi.

kutibu minyoo

unga wa mbegu za mpapai husaidia sana kutibu minyoo katika kuku.

USIKOSE KUTEMBELEA BLOG YETU KUJUA MENGI KUHUSU KUKU.


Wednesday, 26 August 2015

AINA ZA KUKU WA KIENYEJI

Habari ndugu wasomaji wetu,leo tutachambua aina kadhaa za kuku wa kienyeji.Duniani kuna aina karibia 300 za kuku.katika toleo hili tutatazamia aina kubwa tatu za kuku wa kienyeji kibiashara.


1.KUCHI(rhode island)
kuku hawa wana sifa ya kutaga sana mayai na hawasumbuliwi sana na magonjwa pia hua na umbo kubwa sana.


2.CHOTARA(cross hybrid breeds)
Kuku hawa ni wakubwa na wanauzito mkubwa.kuku hawa ni wazuri kwa nyama lakini pia hutaga mayai mengi(10-13) kwa kuku mmoja.(hii si kwa siku moja ni katika mzunguko wa utagaji).kuku hawa ni wazuri kwa biashara huuzwa kuanzia 18,000/= mpaka 25000/= kutokana na mfugaji.




3.KUKU MALAWI 
Kuku hawa ni weusi na pia hua na maumbo makubwa sana,na wanasifa moja ya kutaga mayai mengi sana kuliko kuku wengine.



USIKOSE KUTEMBELEA BLOG YETU KUJUA ZAIDI KUHUSU KUKU WA KIENYEJI

shukrani za dhati.

JE WAJUA,JINSI YA KULEA VIFARANGA?..soma hapa



habari za wakati huu ndugu wasomaji na wafuatiliaji wa blog yetu,leo tutaangalia namna ya kulea vifaranga.zifutazo ni hatua mbali mbali za maandalizi na mapokezi ya vifaranga.

1.MAANDALIZI YA BANDA
banda ni jambo la kwanza kwa mfugaji yoyote.banda la kuku huweza kujengwa kwa matofali,mbao,au hata miti na matope.
mfano wa banda la matofali lenye dirisha kubwa.
Banda la kuku linatakiwa liwe safi wakati wote.


1.Sifa za banda la kuku
lipitishe mwanga wa kutosha
lisiwe na nafasi ya wadudu hatari na hata wanyama kupita
liwe karibu na makazi ya mfugaji
sakafu yake isiwe na matobo tobo mengi(iwe imesakafiwa vizuri kwa njia tofauti)
banda liwe na ukubwa wa kutosha sawa na idadi ya vifaranga.(mita 2 kwa 3)
ndani ya banda kuwepo mabox madogo madogo kwaajili ya kuwekea vifaranga.mabox hutunza joto na chini ya mabox hayo au vitalu kuwepo na pumba za mahindi au mpunga ili kuongeza joto.
mfano wa box hilo katika picha.

2.Andaa vyombo
vyombo kwaajili ya maji na chakula.unaweza kununua vyombo ua ukatumia sahani  za kawaida za nyumbani.kwa maji weka mawe madogo madogo  masafi katika vyombo hivyo ili vifaranga wasitawanye sana maji au wao kuloana na maji hayo.
mfano wa vyombo katika picha


3.Andaa taa ya chemli au bulb
Taa hutumika kwaajili ya kuongeza joto katika box au kitalu cha vifaranga.taa huwekwa ndani ya box hilo.Kwa wafugaji wakubwa hutumia bulb katika mabanda yao.joto katika vifaranga liongezwe wakati wa usiku na mchana liwe la kawaida.



4.Fahamu ratiba na chanjo kwa vifaranga kama ifatavyo.

  • siku 1-5 --dawa ya kufunga vitovu-
  • siku 7 --NEWCASTLE
  • siku 8, 9,10,11--VITAMIN 
  • siku 14--Gomboro
  • Siku ya 15-20-VITAMIN
  • siku 21--gomboro Baada ya hapo endelea na vitamin hadi siku ya 27
  •  Siku ya 28-NEWCASTLE Kisha endelea na vitamin
  • wiki ya 5 chanjo ya ndui
  • wiki ya 6--Ampronium + ctc (siku tano)
  • wiki ya 7--Vitamin
  • wiki ya 8--dawa ya minyoo


ANGALIZO.EPUKA UCHAFU KATIKA BANDA ILI KUEPUSHA MAGONJWA KATIKA BANDA AMBAYO HUPELEKEA KUKU KUUMWA HIVYO KUTAFTIWA DAWA NYINGI ZAIDI NA KUPELEKEA KUONGEZEKA KWA GHARAMA ZA UFUGAJI.

5.CHAKULA

chakula cha kuku kiwe na mchanganyiko ufuatao.

  • nafaka(mahindi,uwele,mtama,ulezi nk)-------kg 40
  • pumba za nafaka_----------------------kg 27
  • chumvi ya jikoni--------------kg 0.5
  • virutubisho----------------------kg 0.05
  • unga wa chokaa na mifupa-----kg 2.25
  • mashudu ya alizeti ufuta au karanga --kg 20
  • dagaa na mabaki ya samaki---kg 10


6.ANDAA KUMBU KUMBU MUHIMU IWE NA;


  • tarehe ya kutotoresha
  • idadi ya vifaranga
  • kiasi cha chakula
  • vifo
  • vifaranga vilivyo uzwa
  • tarehe ya siku ya kurekodi
  • matibabu
  • ugonjwa
  • mfano wa ratiba hiyo



ENDELEA KUFATILIA BLOG HII KUJUA ZAID KUHUSU KUKU WA KIENYEJI
Ahsanteni.




Friday, 21 August 2015

Mawasiliano

Wasiliana nami kwa

No. +255 719 342 444
       +255 718 616 834
Email.  ibrah.tube@gmail.com

Thursday, 20 August 2015

magonjwa ya kuku na jinsi ya kuyadhibiti


habari za wakati huu wapendwa wafugaji na wasio wafugaji,wasomi wa machapisho yetu kwa ujumla.katika toleo hili tunachambua magonjwa mbalimbali ya kuku.magonjwa ya kuku husabibishwa na vitu mbali mbali ikiwemo virusi,minyoo,bakteria,uchafu,wadudu na hata upungufu wa virutubisho katika vyakula vya kuku hawa.magonjwa ambayo husababishwa na virusi hua ni vigumu sana kutibika hivyo mfugaji hushauliwa kuwapa chanjo ya magonjwa hayo.mfano ni mdondo(new castle disease).ugonjwa huu ni hatari sana kwa kua humaliza kuku wengi kwa wakati mmoja.wengine huita huu ugonjwa kideri.
   Mdondo(new castle disease).
kama binadamu aogopavyo ugonjwa wa UKIMWI,basi wafugaji wengi huogopa sana ugonjwa wa mdondo,pia huitwa kideli(newcastle disease).huu ni ugonjwa HATARI unaosababishwa na virusi pia ni ugonjwa huu hauna tiba.Hivyo mfugaji anatakiwa kuwapa chanjo mapema kabla ugonjwa haujafika eneo hilo.dalili za mdondo ni kama.
1.kuku kukohoa au kuhema kwa tabu
2.manyoya ya kuku huvurugika na kua katika hali isiyo ya kawaida.
3.kuku huarisha kinyesi cha kijani
3.kupoteza hamu ya kula na mabawa kupoza
4.kizunguzungu na kuanguka chali
5.kupoteza fahamu

ugonjwa huu hupelekea kuku wengi kufa kufikia hadi asilimia 50 hadi 100 kama usipo dhibitiwa mapema.
Namna ya ugonjwa unavyosambaa
1.virusi hawa huweza kusambaa kwa njia ya hewa au upepo husafirisha virusi hawa.
2.kinyesi cha kuku mwenye mdondo kikikanyagwa na mtu,baiskeli au wanyama wengine na kusafirishwa kwenye banda la kuku,ugonjwa huu huweza pia kusambaa.
3.kuku alie kufa kwa mdondo asipo zikwa vizuri au kuchomwa moto,kuku mzima akila mabaki hayo,kuku hao watakua katika hatari ya kupata mdondo.
JINSI YA KUPAMBANA NA MDONDO
Kama ilivyo elezwa hapo juu,gonjwa hili halina tiba.lakini kuku wakipewa chanjo kwa wakati hua katika usalama.kuna chanjo kama;
1.LASOTA
chanjo hii ni ya vidonge,kidonge kimoja huchanganjwa na maji safi.chanjo hii tolewa baada ya siku tatu kisha rudi baada ya wiki tatu  na rudia kila baada ya majuma manne au kutokana na uonavyo.kabla ya kuku kupewa dawa hii yapaswa wasipewe maji kwa masaa kadhaa kwa siku hio na muda wa kupewa maji basi wapewe sehemu yenye kivuli.
chanjo hii hupatikana katika maduka mbali mbali ya mifugo.
2.Chanjo ya Thermostable 1-2,dawa hii inahuwezo mkubwa wa kustahimili joto,watu wasio na majokofu basi tumia dawa hii ila hifadhi sehem kavu na isio na joto.dawa  hii huweza kukaa wiki mbili baada ya kufunguliwa kwa Mara ya kwanza.
EPUKA YAFUATAYO
kununua kuku katika minada na kuleta bandani
kuruhusu kila mtu kuingia katika banda la kuku
kuacha mabaki ya kuku walikufa ovyo katika mazingira ya kuku
pia,endapo kuku wengi walikufa katika banda hilo basi ni vyema usilete kuku wengine katika banda hilo angalau kwa ,mwezi au zaid.
Tenganisha kuku wenye dalili za ugonjwa na kuku wengine.
ZINGATIA USAFI WA BANDA NA VYOMBO VYA KUKU WAKO.

usikose kutembelea blog hii kwa taarifa nyingine zaidi kuhusu ufugaji wa kuku



Tuesday, 18 August 2015

zijue faida za kuku wa kienyeji

 


   habari za wakati huu wasomaji na wafuatiliaji wa blog yetu.leo ningependa kuchambua faida mbalimbali za kuku wa kienyeji.Imezoeleka katika sehemu nyingi kuku hutumika kama kitoweo,hii ni faida moja wapo ya kuku,lakini pia mayai ya kuku wa asili hua na virutubisho kama Vitamin A,Vitamin E,Vitamin D,vitamin B12,madini ya zinc,madini chuma na pia protein ambayo ni muhimu sana katika ujenzi wa mwili.                                                                                  

   kuku hufugwa kiabishara ni ajira nzuri kwa mfugaji.ufungaji wa kuku huitaji mtaji kidogo katika kuanzisha,pia eneo la dogo.mfano unaweza kuanza na mtaji wa kuku 7,matetea watano na majogoo watatu.kama kuku hawa watapata chakula kilicho bora kuku mmoja huweza kutaga na kutoto hadi vifaranga 12.hivyo kwa matetea watano huweza kufikisha hadi vifaranga 50.mfugaji akiweza kulea Angalau vifaranga 40  ukijumlisha na wale Saba wa mwanzo ni jumla ya kuku 47.kwa idadi hiyo ya kuku inamaana kutakua na ongezeko kubwa la utotoleshaji.kwa wafugaji wasio kua na mtaji mkubwa unaweza kuuza kuku hata kumi kwa bei ya kuanzia 20000/= hadi 25000/=  ambapo huweza kupata laki 2 (200,000/=).fedha hii ikatumika katika kununua chakula na madawa kupambana na magonjwa.kwa njia huu mfugaji huweza hata kufikia kuku 1000 hivyo kufanya mfungaji
kua na mtaji wa 20,000,000.kwa wasio na maeneo ya kutosha ,usiogope biashara hii hujiendesha yenyewe ukianza vizuri unaweza kuuza mayai au kiasi fulani cha kuku ,fedha hiyo ikatumika katika kujiendeleza katika biashara hii.
kuku huliwa kila siku sehemu mbali mbali kama kwenye migahawa,hotelini na kwa mama ntilie hivyo solo lake in la uhakika.
Mali ghafi za kujengea bandana ya kuku hupatikana kirahisi katika sehemu mbali mbali  hata maeneo ya vijijini.Pia vifaa vyake hupatikana katika maduka ya mifugo na huweza kujengwa vifaa vya asili katika maeneo  yasio na maduka hayo.

usikose kutembelea blog hii kwa taarifa nyingine zaidi kuhusu ufugaji wa kuku

Powered by Blogger.

Pages

//]]>