NENO LA USHAWISHI.......JE WEWE NI KIJANA NA UNAPENDA UFUGAJII???somaa hapaa
habari wasomaje na wafuatiliaji wa blog yetu,Leo ningependa kutoa neno la ushawishi kwa vijana wenzangu waliopo shuleni,vyuoni na mtaanii..je ni vipi unatumia muda wako baada ya masomo au kazi???umewahi kupata wazo la biashara??kama umewahi kupata wazo la biashara au la kukuingizia kipato ni kwanini hujaanza mpaka wakati huu???...MAWAZOO.......MAWAZOOO...Mawazo ni mazuri lakini yakifanyiwa kazi,mawazo yasipo fanyiwa kazi hakika kijana mwenzangu utabaki kuvusha tuu na kutamania maisha ya watu wengine.SIRI,siri ya mafanikio yoyote ni kufanya kazi,usiogope mtu mwenyewe mawazo makubwa,ila mheshimu sana mtu anaefanyia kazi mawazo yake.Hivyo siri ni moja,KUFANYA KAZI NA KUJITUMA KATIKA KILA JAMBO UFANYALO.
Saturday, 27 February 2016
JE WAJUA RATIBA YA CHANYO YA KUKU ASILIA/BROILERS??soma hapaaa
HII NI RATIBA YA CHANJO NA DAWA
1. SIKU 1.
Baada ya vifaranga kutotoreshwa
wenye siku moja,vifranga wapewe glucose kwa muda wa masaa 2.Glucose
huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa.baada ya hapo vifaranga
wapewe vitamin mfano ni CHAMPRIX.Pia hii huchanganywa na maji.vifaranga wawe
katika eneo lenye joto na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifanga
wapewe OTC plus(kijiko kimoja cha chai katika lita 5 za maji safi,pia changanya
vitamin.
2.
SIKU YA 7.
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE
(KIDELI).chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kasha
kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga
mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya
hapo vifaranga wapewe maji yenye vitamin
mfano wa vifaranga wenye wiki moja(siku saba).Hawa wamepata chanjo ya newcastle na kama utakavyoona katika video hapa chini vifaranga wamechangamka.
3.
SIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD).chanjo hii
pia huchanganywa katika maji na kupewe vifaranga kwa muda wa masaa mawili
tu.baada ya hapo vifaranga wepewe vitamin.
4.
Siku ya 21.(wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle
5.
SIKU 28(mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD
6. SIKU 35(mwezi 1 na wiki 1)
Kipindi hiki kuku wapewe vitamin ya kutosha.
7. WIKI YA 6-8
KUKU wapatiwe kinga ya ndui (fowl
pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asie na utaalam kuwapa kuku,tafta mtaalum
kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.
8.
WIKI YA 8
Kuku
wapatiwe dawa ya minyoo na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle