Saturday, 30 September 2017

Tabia za kuku mgonjwa




 Kuku asie na afya huonesha hizi dalili.
l   kuku huchoka na kupoteza furaha
l   macho yaliofifi na upanga legevu
l   Hulala na kusinzia wakati wote
l   Hula na kunywa kidogo
l   Hupunguza kutaga mayai
l   Hushusha manyoya na manyoya hutimka
l   Kinyesi chenye maji maji  na mara nyingine damu au minyoo
l   Kuku hukohoa na kupumua kwa tabu sana

Wednesday, 27 September 2017

MAPUNGUFU YA KUKU ASILIA NA CHANGAMOTO ZAKE

Mapungufu ya Kuku wa Asili:
Hutaga mayai madogo wastani wa gramu 47 ambapo kuku wa kisasa wastani wa gramu 55,aidha hutaga mayai machache wastani wa mayai 60 kwa mwaka ambapo kuku wa kisasa huweza kutaga hadi mayai 300 kwa mwaka.(CHOTARA NA KROILERS HUTAGA MAYAI 240-260 KWA MWAKA)
Ukuaji taratibu – kuku wa asili hukua taratibu kutokana na lishe duni. Kutokana na hali hiyo kuku
huchukua muda mrefu (miezi sita) kufikia uzito wa kuchinjwa (kilo 1 - 1.5). Hali hii pia hufanya faida ya ufugaji wa kuku wa asili kuchukua muda mrefu kupatikana.
Nyama yake ni ngumu (huchukua muda mrefu kuiva) ikilinganishwa na kuku wa kisasa.

Changamoto katika ufugaji kuku wa asili:
1. Mabanda: Ukosefu wa mabanda bora.
2. Wezi, wanyama na ndege hushambulia kuku.
3. Magonjwa: kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku.
4. Tabia na miiko ya baadhi ya jamii. Baadhi ya jamii za makabila hapa nchini huona ufugaji wa kuku kama ni kitu duni.
5. Upatikanaji haba wa chanjo za magonjwa kama vile, mdondo, ndui, homa ya matumbo.

6. Si rahisi kuweza kupata kabila halisi (Pure breed) au kizazi halisi (Pure line) za kuku wa Asili
7. kutokana na mazingira ya muingiliano wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo
8. kuku hawa wana tofauti za kimaumbile zilizosababisha kuwepo kwa kabila mbalimbali baina yao.
9. Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku hao wanakotoka.
10. Kutokana na muingiliano wa vizazi, maumbile hayo yanaweza yakajitokeza kwenye aina mbalimbali za kuku, ikiwa na maana kwamba kuku mmoja kuwa na kabila moja au zaidi kwa mara moja. Hivyo aina za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa Asili kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.

Sunday, 27 August 2017

sifa za mayai bora kwaaajili ya kutotolesha katika mashine za kutotolesha(incubator)

Habari za wakati huu wasoma na wafuatiliaje wa mtandao wetu unaolenga katika kuelimisha watu hasa vijana katika ufugaji wa kuku wa kienyeji na chotara,Hivi karibuni watu wengi wamekua wakilalamika juu ya utotoleshaji mbovu wengi wamekua wikidhani ni mashine za kutotolesha,lakini tatizo kubwa ni sisi wafugaji kushindwa kutunza mayai vizuri,Hapa chini ni maelezo ya namna bora ya kutunza mayai kwaajili ya kutotolesha.



MAMBO MUHIMU KWA  YAI KUWEZA KUTOTOLESHWA
·        

       Yai lisizidi siku 7 mpaka 8 tangu litagwe

·        






Mayai yahifadhiwe kwenye trei yakitoka kuokotwa bandani

·         Zingatia Uwiano mzuri wa majogoo kwa matetea (1:8-10)

·         Mayai ya mtago wa kwanza sio mazuri kwa kutotolesha

·         Mayai ya kuku mzee sio mazuri kwa kutotolesha

·         Kuku watagaji wanapaswa kupewa chakula bora na cha kutosha

·         Mayai yahifadhiwe sehemu isio na joto kali

·         Mayai machafu hayafai kwa kutotolesha

·         Mayai madogo sana hayafai kwa kutotolesha

·         Mayai yenye kreki(nyufa)hayafai kwa kutotolesha

·         Mayai yenye umbo kubwa sana hayafai kwa kutotolesha

·         Mayai yenye viini viwili hayafai kwa kutotolesha

·         Yai lisihifadhiwe kwenye friji(hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isio na joto)

·         Wakati unahifadhi mayai katika trei hakikisha sehemu ya yai iliyochongoka inaangalia chini


·         Tengeneza viota kwaajili ya kuku kutagia ili kuepusha mayai yalio machafu.






KWA MAWASILIANO TUPIGIE KWA NUMBER ZIFUATAZO
0719342444/0788337971

0718616834

Wednesday, 7 June 2017

SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU

SIFA ZA BANDA BORA.
Katika mazingira yetu ya kawaida kuku hutaga katika viota na kupumzika katika vivuli na kutumia mda mwingine kujitafutia chakula. Kuku hutumia muda wake mwingi katika kujitafutia chakula katika ardhi na sehemu za chakula.Katika ufugaji wetu wa asili kuku hufungiwa katika nyumba zao nyakati za usiku na kufunguliwa asubuhi ila wakajitafutie chakula,Baadhi ya wafugaji wameboresha hii na kufuga kibiashara ambapo kuku hawa hufungwa ndani na kupewa chakula, hivyo katika ufugaji wa kuku,banda au nyumba ya kuku ni muhimu ili kuepesha wizi,hali mbaya ya hewa,wadudu na hata wanyama wakali.
Kuku wanaotaga huchagua sehemu za kutaga,kuku huchagua sehemu ilio kimya na ilio fichika,sehemu hiyo iwe na ukubwa wa wastani. (mchemraba wa 40 cm),sehemu iwe na giza kwa mbali .Kabla ya kutaga kuku hufanya tathmini ya mambo mbali mbalikatika kipindi hiki tetea hutoa sauti kuonesha anatafuta sehemu ya kutaga,na akipata sehemu ya kutagia na kutaga yai pia hutoa sauti nyingine kama ishara ya kijipongeza.(pride of achievement call)
 Vitu muhimu katika banda/nyumba ya kuku ni:
  • Eneo la kutosha kuku kulingana na idadi;
  • Madirisha makubwa kwaajili ya kupitisha hewa;
  • Mwanga wa kutosha;
  • Banda liwe na ulinzi na usalama kutoka kwa wadudu wa wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku
.
Eneo: uwiano wa kuku katika eneo
Hili ni jambo la msingi sana kulijua katika kuandaa banda la kuku kutokana na idadi ya kuku unaotaka kuwafuga.eneo litaamua ni idadi gani ya kuku wafugwe.kwa mfano kwa nyumba ya vipimo,6 m kwa 11 m inaweza kuchukua kuku wanao taga hadi 200,Kwa kila kuku watatu watakaa huru zaidi katika eneo lenye mita moja ya mraba(one square meter).

 JEDWALI:
AINA YA KUKU
ENEO LA SAKAFU
(idadi ya kuku/m
2)
Eneo la kutagia
(kwa tetea mmoja)
Kuku wa mayai
3
25 cm (10 in)
Kuku chotara(mayai&nyama)
4
20 cm (8 in)
Kuku wa nyama
4-5
15-20 cm (6-8 in)
Kuku wakiwa katika eneo pungufu na vipimo huanza kuonesha tabia zisizo kawaida mfano kudonoana na pia magonjwa husambaa kwa urahisi,na endapo eneo litakua kubwa sana pia kuku huweza kuonesha tabia zisizo kawaida.Banda bora husaidia kupata mazao bora.

 Uingizaji hewa:
Mzunguko wa hewa ni muhimu sana katika mambo ya kuzingatia katika ujenzi wa banda la kuku,Nyumba ya kuku yenye madirisha pande zote hua ni bora zaidi au madirisha makubwa.
Joto katika banda ni muhimu sana ili kuongeza uzalishaji pia joto likizidi huweza kupelekea kifo.Kuku huweza kuvumilia baridi chini ya nyuzi joto 10 lakini hupata tabu sana nyuzi joto likizidi 40.Kuku hana uwezo wa kutoa jasho kutokana na maumbile yake.Kuku hupunguza joto kwa njia ya kupumua(cool themselves by panting out water in their breath),njia hii ya kupunguza joto kwa kuku haina ufanisi sana endapo joto litazidi nyuzi joto 46 na kuendelea.Hivyo basi nyumba ya kuku iwe na paa lililo nyanyuka ili kuweza kuruhusu mzunguko mkubwa wa hewa na pia kupunguza joto.
Joto likizidi katika banda la kuku yafuatayo hujitokeza.
  • Kuongezeka kwa joto hupelekea kuku kupunguza kula hasa chakula kikavu;
  • Kuku hunywa maji mengi kujaribu kupunguza joto;
  • Kiwango cha ukuaji hupungua kwa kuku; and
  • Hupunguza kutaga,majogoo hushindwa kutoa mbegu bora,vifaranga hutoka walio dhaifu

Mwanga katika banda la kuku.
Katika ujenzi wa banda la kuku ni muhimu kuzingatia kiasi cha mwanga na miale ya jua inayoingia katika banda,mwanga unatakiwa kuwa wa kutosha.angalia picha hapa chini ili kujua namna ya kujenga banda la kuku,

Wednesday, 31 May 2017

jifunze kutengeneza chakula cha kuku,nguruwe,na ng'ombe kwa teknolojia ya hydroponics

SEHEMU YA KWANZA
Tumerahisisha zaidi maelezo na kuifanya iakisi mazingira harisi ya mfugaji wa kitanzania
Hydroponic ni nini?
Ni mbinu ya kukuza mimea kwa kutumia mchanganyiko wa virutubisho vya madini katika maji bila kutumia udongo. Mchakato huu huchukua siku 6 hadi tisa kukamilika.
Kilo moja ya mbegu huzalisha wastani wa kilo 6 hadi kumi za majani na mizizi.



Faida za Teknolojia hii
i. Malisho huzalishwa ndani ya muda mfupi katika eneo dogo.mfano eneo la 4X3 mita huweza kutoa malisho sawa na ekari 2.
ii. Chakula hiki hulika chote kwa mifugo. Wanakula najani yote pamoja na mizizi. Hakuna upotevu wa chakula.
iii. Mahitaji ya maji ni madogo na maji yanaweza kutumika tena na tena.
iv. Gharama za uendeshaji wake ni mdogo; hakuna kuandaa ardhi, palizi na gharama za uvunaji.
v. Uwezekano mdogo sana wa wadudu ama magonjwa kushambulia.
Faida katika ulishaji
i. Chakula hiki ni laini hivyo mmengényo wake katika mifugo ni mkubwa hivyo sehemu kubwa hutumika katika mwili wa mifugo na uzalishaji.
ii. Mazao ya mifugo uboreka zaidi na kuendana na mahtaji ya soko. Mfano:
mayai ya kuku huwa na kiini cha njano zaidi wanapokula majani.
Maziwa huwa na uwiano mzuri wa Omega 3 na Omega 6 amino acid ambazo hujenga afya imara ya mlaji.
iii. Hupunguza gharama za chakula na hivyo kuongeza faida.
iv. Virutubisho vingi hasa vitamin ambazo huchangia afya ya mifugo kuimalika.
v. Kinapolishwa kwa mchanganyiko na vyakula vingine kwa uwiano tutakaoutoa hapo mbele, uzalishaji na ukuaji wa mifugo huwa mzuri zaidi.




Vifaa mihimu
Sehemu/chumba cha kukuzia.
Nguzo na fito za kutengeneza chanja kwa ajili ya kupanga trei.









 Trei za plastiki/aluminiamu.









 Dawa yenye Chlorine (kama Waterguard) ama JIK kuua vijidudu katika maji na mbegu.
Virutubisho (nutrients): wengine hutumia buster za mazao (hakikisha haina madhara kwa mifugo).









 Pump (sprayer) kunyunyiza maji.
Mbegu.


Mbegu zinazoweza kutumika
 Shayiri, mahindi, ngano, mtama na nafaka nyingine nyingi.



SEHEMU YA PILI


UZALISHAJI WA MALISHO KWA TEKNOLOJIA YA HYDROPONIC
SEHEMU YA PILI

HATUA KWA HATUA KATIKA KUZALISHA HYDROPONIC
Kwa kufata hata hizi unaweza kuzalisha malisho yako mwenyewe nyumbani.
1. Chagua mbegu ambazo hazijaanza kuchipua, na hazina kemikali ama dawa ya aina yoyote.
2. Loweka mbegu katika mchanganyiko wa maji na Chlorine kwa masaa mawili kuepusha kuvu/uvundo ama vimelea vya magonjwa kumea na kukua.
3. Zitoe mbegu kwenye maji, zioshe kisha ziloweke kwenye maji safi kwa masaa 24 kuwezesha mbegu kufyonza maji vema.
4. Katika kupanda mbegu, pima kilo mbili za mbegu kwa kila trei yenye urefu wa Cm 80 kwa upana wa  Cm 40.
5. Sambaza mbegu kwenye trei kwa usawa, (zisizidi Cm 3 kimo) ili kuwe na nafasi ya kutosha kwa kila mbegu kuchipua (kuota).
6. Hakikisha trei zina matundu kwenye kitako (chini) ambayo yamesambaa kwa usawa kuwezesha maji ya ziada kutoka.
7. Hamishia trei kwenye chanja ulizotengeneza. Mbegu zitaanza kuota katika hatua hii. Fanya hii ni siku ya kwanza.
8. Nyunyizia maji (kwa pampu) toka siku ya kwanza hadi ya sita, kwa mara nne katika kila masaa 24.

ZINGATIA.
Mbegu zenye dawa au sumu yoyote ni hatari kwa wanyama. zinaweza kuwadhoofisha ama kuwaua. hakikisha hautumii mbegu zenye dawa.

Jinsi ya kulisha

Kuku: kwa kuku 100 wanaotaga (layer) wape kilo 8  za hydroponics na waongezee kilo 4 za chakula cha layer (layer mash) kwa siku.

Nguruwe: katika unenepeshaji wape kilo 2 za hydroponics na 1.5 za chakula kikavu (nafaka) kwa nguruwe mmoja kwa siku.

Ngómbe, mbuzi: wanaweza kutegemea majani haya tu na kuwa na uzalishaji mzuri bila nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka. Kama uzalishaji wa maziwa ni mkubwa sana (zaidi ya lita 12 kwa siku) ni vema kuwaongezea nafaka.

Sungura: wanaweza kutegemea majani haya tu lakini ni vema kuwapa nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka (angalau kwa uwiano wa 50%).

MAJIBU YA MASWALI.
TREI: wengi mliuliza kuhusu upatikanaji wa trei. Trei tumeagiza na bei ni shilingi elfu saba moja. Weka oda mapema katika namba chini.
NUTRIENTS: wengine mliuliza kuhusu mbolea. mbelea ni adimu na bei kubwa. kwa uchunguzi tulioufanya BOOSTER ya mimea hasa yenye NPK inaweza kutumika kama mbadala wa nutrients. kama tulivyoeleza kwenye sehemu ya kwanza. booster ichanganywe na maji kabla ya kumwagilia.
matumizi ya nyungo. unaweza kutumia ungo kupanda hyadroponi. ila ni ghali kwa sababu ungo huoza haraka sababu ya unyevunyevu wakati wote. ivyo ni muhimu kununua trei zinazodumu siku zote.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na kuweka order ya trei : 0755639835


Monday, 27 February 2017

PATA VIFARANGA CHOTARA,ANZA KUFUGA LEO

Habari wapenzi wasomaji wetu,Leo napenda kuwaletea biashara ya vifaranga wa kuku chotara.Vifaranga wa mwezi mmoja wakiwa na chanjo kama
1.NEWCASTLE
2.GUMBORO
3. NDUI,

Pia wanunuzi wa vifaranga watapewa semina fupi kabla ya kupewa vifaranga.



Picha ya hapa chini ni baadhi ya vifaranga chotara wakina na mwezi mmoja.


Picha ya hapa chini ni vifaranga wa siku moja




Vifaranga hapa chini ni vifaranga wa wiki moja


 Wafugaji kutoka KUKUTAJIRI katika kazi ya ukusanyaji mayai kwaajili ya kwenda kutotolesha,je unajua sifa ya mayai bora kwaajili ya kutotolesha?endelea kufuatilia mtandao wetu utajifunza sifa hizo.

hapa chini ni kuku walezi kwaajili ya utagaji mayai ili yakatotoleshwe 

hapa chini ni aina ya jogoo kutoka kukutajiri.


kuku wazazi wakipewa chakula na wafugaji kutoka kukutajiri

bei ya vifaranga ni;
VIFANGA WA MWEZI NI TSH 4000/=
VIFARANGA WA SIKU NI TSH 2000/=
wasiliana nasi kwa namba 0719342444 au 0718616834

Powered by Blogger.

Pages

//]]>