Wednesday, 7 June 2017

SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU

SIFA ZA BANDA BORA.
Katika mazingira yetu ya kawaida kuku hutaga katika viota na kupumzika katika vivuli na kutumia mda mwingine kujitafutia chakula. Kuku hutumia muda wake mwingi katika kujitafutia chakula katika ardhi na sehemu za chakula.Katika ufugaji wetu wa asili kuku hufungiwa katika nyumba zao nyakati za usiku na kufunguliwa asubuhi ila wakajitafutie chakula,Baadhi ya wafugaji wameboresha hii na kufuga kibiashara ambapo kuku hawa hufungwa ndani na kupewa chakula, hivyo katika ufugaji wa kuku,banda au nyumba ya kuku ni muhimu ili kuepesha wizi,hali mbaya ya hewa,wadudu na hata wanyama wakali.
Kuku wanaotaga huchagua sehemu za kutaga,kuku huchagua sehemu ilio kimya na ilio fichika,sehemu hiyo iwe na ukubwa wa wastani. (mchemraba wa 40 cm),sehemu iwe na giza kwa mbali .Kabla ya kutaga kuku hufanya tathmini ya mambo mbali mbalikatika kipindi hiki tetea hutoa sauti kuonesha anatafuta sehemu ya kutaga,na akipata sehemu ya kutagia na kutaga yai pia hutoa sauti nyingine kama ishara ya kijipongeza.(pride of achievement call)
 Vitu muhimu katika banda/nyumba ya kuku ni:
  • Eneo la kutosha kuku kulingana na idadi;
  • Madirisha makubwa kwaajili ya kupitisha hewa;
  • Mwanga wa kutosha;
  • Banda liwe na ulinzi na usalama kutoka kwa wadudu wa wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku
.
Eneo: uwiano wa kuku katika eneo
Hili ni jambo la msingi sana kulijua katika kuandaa banda la kuku kutokana na idadi ya kuku unaotaka kuwafuga.eneo litaamua ni idadi gani ya kuku wafugwe.kwa mfano kwa nyumba ya vipimo,6 m kwa 11 m inaweza kuchukua kuku wanao taga hadi 200,Kwa kila kuku watatu watakaa huru zaidi katika eneo lenye mita moja ya mraba(one square meter).

 JEDWALI:
AINA YA KUKU
ENEO LA SAKAFU
(idadi ya kuku/m
2)
Eneo la kutagia
(kwa tetea mmoja)
Kuku wa mayai
3
25 cm (10 in)
Kuku chotara(mayai&nyama)
4
20 cm (8 in)
Kuku wa nyama
4-5
15-20 cm (6-8 in)
Kuku wakiwa katika eneo pungufu na vipimo huanza kuonesha tabia zisizo kawaida mfano kudonoana na pia magonjwa husambaa kwa urahisi,na endapo eneo litakua kubwa sana pia kuku huweza kuonesha tabia zisizo kawaida.Banda bora husaidia kupata mazao bora.

 Uingizaji hewa:
Mzunguko wa hewa ni muhimu sana katika mambo ya kuzingatia katika ujenzi wa banda la kuku,Nyumba ya kuku yenye madirisha pande zote hua ni bora zaidi au madirisha makubwa.
Joto katika banda ni muhimu sana ili kuongeza uzalishaji pia joto likizidi huweza kupelekea kifo.Kuku huweza kuvumilia baridi chini ya nyuzi joto 10 lakini hupata tabu sana nyuzi joto likizidi 40.Kuku hana uwezo wa kutoa jasho kutokana na maumbile yake.Kuku hupunguza joto kwa njia ya kupumua(cool themselves by panting out water in their breath),njia hii ya kupunguza joto kwa kuku haina ufanisi sana endapo joto litazidi nyuzi joto 46 na kuendelea.Hivyo basi nyumba ya kuku iwe na paa lililo nyanyuka ili kuweza kuruhusu mzunguko mkubwa wa hewa na pia kupunguza joto.
Joto likizidi katika banda la kuku yafuatayo hujitokeza.
  • Kuongezeka kwa joto hupelekea kuku kupunguza kula hasa chakula kikavu;
  • Kuku hunywa maji mengi kujaribu kupunguza joto;
  • Kiwango cha ukuaji hupungua kwa kuku; and
  • Hupunguza kutaga,majogoo hushindwa kutoa mbegu bora,vifaranga hutoka walio dhaifu

Mwanga katika banda la kuku.
Katika ujenzi wa banda la kuku ni muhimu kuzingatia kiasi cha mwanga na miale ya jua inayoingia katika banda,mwanga unatakiwa kuwa wa kutosha.angalia picha hapa chini ili kujua namna ya kujenga banda la kuku,

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Pages

//]]>