SIFA ZA BANDA BORA.
Katika mazingira yetu ya kawaida kuku hutaga
katika viota na kupumzika katika vivuli na kutumia mda mwingine kujitafutia chakula. Kuku hutumia muda wake mwingi katika kujitafutia chakula katika ardhi na
sehemu za chakula.Katika ufugaji wetu wa asili kuku hufungiwa katika nyumba zao
nyakati za usiku na kufunguliwa asubuhi ila wakajitafutie chakula,Baadhi ya
wafugaji wameboresha hii na kufuga kibiashara ambapo kuku hawa hufungwa ndani
na kupewa chakula, hivyo katika ufugaji wa kuku,banda au nyumba ya kuku ni
muhimu ili kuepesha wizi,hali mbaya ya hewa,wadudu na hata wanyama wakali.
Kuku wanaotaga huchagua sehemu za kutaga,kuku
huchagua sehemu ilio kimya na ilio fichika,sehemu hiyo iwe na ukubwa wa
wastani. (mchemraba wa 40 cm),sehemu iwe na giza kwa mbali .Kabla ya kutaga
kuku hufanya tathmini ya mambo mbali mbalikatika kipindi hiki tetea hutoa sauti
kuonesha anatafuta sehemu ya kutaga,na akipata sehemu ya kutagia na kutaga yai
pia hutoa sauti nyingine kama ishara ya kijipongeza.(pride of achievement call)
Vitu muhimu katika banda/nyumba ya kuku ni:
- Eneo
la kutosha kuku kulingana na idadi;
- Madirisha makubwa kwaajili ya kupitisha hewa;
- Mwanga
wa kutosha;
- Banda
liwe na ulinzi na usalama kutoka kwa wadudu wa wanyama wanaoweza kuwadhuru
kuku
.
Eneo: uwiano wa kuku katika eneo
Hili ni jambo la msingi sana kulijua katika
kuandaa banda la kuku kutokana na idadi ya kuku unaotaka kuwafuga.eneo litaamua
ni idadi gani ya kuku wafugwe.kwa mfano kwa nyumba ya vipimo,6 m kwa 11 m
inaweza kuchukua kuku wanao taga hadi 200,Kwa kila kuku watatu watakaa huru
zaidi katika eneo lenye mita moja ya mraba(one square meter).
JEDWALI:
AINA YA KUKU
|
ENEO
LA SAKAFU
(idadi ya kuku/m2) |
Eneo
la kutagia
(kwa tetea mmoja) |
Kuku wa mayai
|
3
|
25
cm (10 in)
|
Kuku chotara(mayai&nyama)
|
4
|
20
cm (8 in)
|
Kuku wa nyama
|
4-5
|
15-20
cm (6-8 in)
|
Kuku wakiwa katika eneo pungufu na vipimo huanza
kuonesha tabia zisizo kawaida mfano kudonoana na pia magonjwa husambaa kwa
urahisi,na endapo eneo litakua kubwa sana pia kuku huweza kuonesha tabia zisizo
kawaida.Banda bora husaidia kupata mazao bora.
Uingizaji
hewa:
Mzunguko wa hewa ni muhimu sana katika mambo ya
kuzingatia katika ujenzi wa banda la kuku,Nyumba ya kuku yenye madirisha pande
zote hua ni bora zaidi au madirisha makubwa.
Joto katika banda ni muhimu sana ili kuongeza
uzalishaji pia joto likizidi huweza kupelekea kifo.Kuku huweza kuvumilia baridi
chini ya nyuzi joto 10 lakini hupata tabu sana nyuzi joto likizidi 40.Kuku hana
uwezo wa kutoa jasho kutokana na maumbile yake.Kuku hupunguza joto kwa njia ya
kupumua(cool themselves by panting out water in their breath),njia hii ya
kupunguza joto kwa kuku haina ufanisi sana endapo joto litazidi nyuzi joto 46
na kuendelea.Hivyo basi nyumba ya kuku iwe na paa lililo nyanyuka ili kuweza
kuruhusu mzunguko mkubwa wa hewa na pia kupunguza joto.
Joto likizidi katika banda la kuku yafuatayo
hujitokeza.
- Kuongezeka
kwa joto hupelekea kuku kupunguza kula hasa chakula kikavu;
- Kuku
hunywa maji mengi kujaribu kupunguza joto;
- Kiwango
cha ukuaji hupungua kwa kuku; and
- Hupunguza
kutaga,majogoo hushindwa kutoa mbegu bora,vifaranga hutoka walio dhaifu
Mwanga katika banda la kuku.
Katika ujenzi wa banda la kuku ni muhimu kuzingatia kiasi cha mwanga na miale ya jua inayoingia katika banda,mwanga unatakiwa kuwa wa kutosha.angalia picha hapa chini ili kujua namna ya kujenga banda la kuku,
0 comments:
Post a Comment