Habari za wakati huu wasoma na wafuatiliaje wa mtandao wetu unaolenga katika kuelimisha watu hasa vijana katika ufugaji wa kuku wa kienyeji na chotara,Hivi karibuni watu wengi wamekua wakilalamika juu ya utotoleshaji mbovu wengi wamekua wikidhani ni mashine za kutotolesha,lakini tatizo kubwa ni sisi wafugaji kushindwa kutunza mayai vizuri,Hapa chini ni maelezo ya namna bora ya kutunza mayai kwaajili ya kutotolesha.
Yai lisizidi siku 7 mpaka 8 tangu litagwe
MAMBO MUHIMU KWA YAI KUWEZA KUTOTOLESHWA
·
Yai lisizidi siku 7 mpaka 8 tangu litagwe
·
Zingatia Uwiano mzuri wa majogoo kwa matetea
(1:8-10)
·
Mayai ya mtago wa kwanza sio mazuri kwa
kutotolesha
·
Mayai ya kuku mzee sio mazuri kwa kutotolesha
·
Kuku watagaji wanapaswa kupewa chakula bora na
cha kutosha
·
Mayai yahifadhiwe sehemu isio na joto kali
·
Mayai machafu hayafai kwa kutotolesha
·
Mayai madogo sana hayafai kwa kutotolesha
·
Mayai yenye kreki(nyufa)hayafai kwa kutotolesha
·
Mayai yenye umbo kubwa sana hayafai kwa
kutotolesha
·
Mayai yenye viini viwili hayafai kwa kutotolesha
·
Yai lisihifadhiwe kwenye friji(hifadhi sehemu
yenye hewa ya kutosha na isio na joto)
KWA MAWASILIANO TUPIGIE KWA NUMBER
ZIFUATAZO
0719342444/0788337971
0718616834