Magonjwa ya kuku kwa ujumla yapo mengi sana na kuna baadhi
ya magonjwa ambayo hayapo hapa nchini,ni vyema kujua dalili hizi za magonjwa
mapema ili kuepusha hasara inayoweza kutokea kutokana na vifo ambavyo
huchangiwa na magonjwa haya.
Dalili hizo
kwa ujumla ni kama ifuatavyo
1.
Kuku
kupoteza hamu ya kula
2.
Kuku
kuzubaa na kukaa sehemu moja kwa muda mrefu
3.
Kushuka
kwa kiwango cha utagaji
4.
Vifaranga
kudumaa
5.
Macho
kua mekundu
6.
Kujikunja
shingo
7.
Kutetemeka,kutoa
maji maji puani,mdomoni na machoni
8.
Kutoa
kinyesi chenye rangi ya kijani,au kinyesi kilicho changanyika na damu au
cheupe.
9.
Kukohoa
10. Kukonda
Endapo kuku
wako ataonesha mojawapo ya dalili hizo basi mfugaji itamlazimu kutafta daktari
wa mifugo au kuku wapatiwe dawa.kujua
madawa mbali mbali ya tazama post nyingine katika blog hii.Pia unaweza
kufatilia mambo mbalimbali kuhusu kuku kupitia ukurasa wetu wa INSTAGRAM kwa
jina la kukutajiri.