Wednesday, 26 August 2015



habari za wakati huu ndugu wasomaji na wafuatiliaji wa blog yetu,leo tutaangalia namna ya kulea vifaranga.zifutazo ni hatua mbali mbali za maandalizi na mapokezi ya vifaranga.

1.MAANDALIZI YA BANDA
banda ni jambo la kwanza kwa mfugaji yoyote.banda la kuku huweza kujengwa kwa matofali,mbao,au hata miti na matope.
mfano wa banda la matofali lenye dirisha kubwa.
Banda la kuku linatakiwa liwe safi wakati wote.


1.Sifa za banda la kuku
lipitishe mwanga wa kutosha
lisiwe na nafasi ya wadudu hatari na hata wanyama kupita
liwe karibu na makazi ya mfugaji
sakafu yake isiwe na matobo tobo mengi(iwe imesakafiwa vizuri kwa njia tofauti)
banda liwe na ukubwa wa kutosha sawa na idadi ya vifaranga.(mita 2 kwa 3)
ndani ya banda kuwepo mabox madogo madogo kwaajili ya kuwekea vifaranga.mabox hutunza joto na chini ya mabox hayo au vitalu kuwepo na pumba za mahindi au mpunga ili kuongeza joto.
mfano wa box hilo katika picha.

2.Andaa vyombo
vyombo kwaajili ya maji na chakula.unaweza kununua vyombo ua ukatumia sahani  za kawaida za nyumbani.kwa maji weka mawe madogo madogo  masafi katika vyombo hivyo ili vifaranga wasitawanye sana maji au wao kuloana na maji hayo.
mfano wa vyombo katika picha


3.Andaa taa ya chemli au bulb
Taa hutumika kwaajili ya kuongeza joto katika box au kitalu cha vifaranga.taa huwekwa ndani ya box hilo.Kwa wafugaji wakubwa hutumia bulb katika mabanda yao.joto katika vifaranga liongezwe wakati wa usiku na mchana liwe la kawaida.



4.Fahamu ratiba na chanjo kwa vifaranga kama ifatavyo.

  • siku 1-5 --dawa ya kufunga vitovu-
  • siku 7 --NEWCASTLE
  • siku 8, 9,10,11--VITAMIN 
  • siku 14--Gomboro
  • Siku ya 15-20-VITAMIN
  • siku 21--gomboro Baada ya hapo endelea na vitamin hadi siku ya 27
  •  Siku ya 28-NEWCASTLE Kisha endelea na vitamin
  • wiki ya 5 chanjo ya ndui
  • wiki ya 6--Ampronium + ctc (siku tano)
  • wiki ya 7--Vitamin
  • wiki ya 8--dawa ya minyoo


ANGALIZO.EPUKA UCHAFU KATIKA BANDA ILI KUEPUSHA MAGONJWA KATIKA BANDA AMBAYO HUPELEKEA KUKU KUUMWA HIVYO KUTAFTIWA DAWA NYINGI ZAIDI NA KUPELEKEA KUONGEZEKA KWA GHARAMA ZA UFUGAJI.

5.CHAKULA

chakula cha kuku kiwe na mchanganyiko ufuatao.

  • nafaka(mahindi,uwele,mtama,ulezi nk)-------kg 40
  • pumba za nafaka_----------------------kg 27
  • chumvi ya jikoni--------------kg 0.5
  • virutubisho----------------------kg 0.05
  • unga wa chokaa na mifupa-----kg 2.25
  • mashudu ya alizeti ufuta au karanga --kg 20
  • dagaa na mabaki ya samaki---kg 10


6.ANDAA KUMBU KUMBU MUHIMU IWE NA;


  • tarehe ya kutotoresha
  • idadi ya vifaranga
  • kiasi cha chakula
  • vifo
  • vifaranga vilivyo uzwa
  • tarehe ya siku ya kurekodi
  • matibabu
  • ugonjwa
  • mfano wa ratiba hiyo



ENDELEA KUFATILIA BLOG HII KUJUA ZAID KUHUSU KUKU WA KIENYEJI
Ahsanteni.




Related Posts:

  • Dalili za jumla za magonjwa ya kuku...soma hapa kujua dalili hizo.. Magonjwa ya kuku kwa ujumla yapo mengi sana na kuna baadhi ya magonjwa ambayo hayapo hapa nchini,ni vyema kujua dalili hizi za magonjwa mapema ili kuepusha hasara inayoweza kutokea kutokana na vifo ambavyo huchangiwa na mag… Read More
  • DALILI ZA JUMLA ZA KUKU Magonjwa ya kuku kwa ujumla yapo mengi sana na kuna baadhi ya magonjwa ambayo hayapo hapa nchini,ni vyema kujua dalili hizi za magonjwa mapema ili kuepusha hasara inayoweza kutokea kutokana na vifo ambavyo huchangiwa na mago… Read More
  • TANZANIA YA KILIMO,VIJANA TURUDI MASHAMBANIHabari za wakati huu wapenzi wasomaji wetu,Leo ningependa kutoa mawazo yangu kuhusu suala la kilimo nchini. Tanzania ni nchi maskini,uchumi wa nchi hii unategemea zaidi kilimo.Kilimo huchangia asilimia 50 ya pato la ndani la … Read More
  • RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA Kuku chotara/kienyeji hufungwa kwa matumizi ya kutaga mayai na pia kwa nyama.Mfugaji atachagua aina na mfumo wa chakula kutokana na yeye anafuga kuku hawa kwa matumizi gani. Ili kuku wafugwe kwaajili ya mayai fuata ratib… Read More
  • JE WAJUA,JINSI YA KULEA VIFARANGA?..soma hapa habari za wakati huu ndugu wasomaji na wafuatiliaji wa blog yetu,leo tutaangalia namna ya kulea vifaranga.zifutazo ni hatua mbali mbali za maandalizi na mapokezi ya vifaranga. 1.MAANDALIZI YA BANDA banda ni jambo la kwanza… Read More

1 comment:

watembeleaji

A visitor from Rostov-on-don viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 4 hrs 45 mins ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 1 day 5 hrs ago
A visitor from Gauteng viewed 'JE WAJUA,JINSI YA KULEA VIFARANGA?..soma hapa ~ fa' 2 days ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 4 days ago
A visitor from Nuremberg viewed '2015 ~ fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 4 days 15 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 6 days 22 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 7 days 19 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'sifa za mayai bora kwaaajili ya kutotolesha katika' 8 days 6 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 8 days 19 hrs ago
A visitor from Mbeya viewed 'KUKU CHOTARA NA TABIA ZAKE ~ fahamu uleaji wa kuku' 11 days 5 hrs ago

Sample Text

Powered by Blogger.

Pages

watembeleaji wa mtandao wetu

A visitor from Rostov-on-don viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 4 hrs 45 mins ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 1 day 5 hrs ago
A visitor from Gauteng viewed 'JE WAJUA,JINSI YA KULEA VIFARANGA?..soma hapa ~ fa' 2 days ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 4 days ago
A visitor from Nuremberg viewed '2015 ~ fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 4 days 15 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 6 days 22 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 7 days 19 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'sifa za mayai bora kwaaajili ya kutotolesha katika' 8 days 6 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 8 days 19 hrs ago
A visitor from Mbeya viewed 'KUKU CHOTARA NA TABIA ZAKE ~ fahamu uleaji wa kuku' 11 days 5 hrs ago

Popular Posts

kukutajiri on facebook

fuatilia makala zetu kupitia facebook kupitia ukurasa wetu wenye jina la hapo juu
//]]>