Thursday 27 October 2016

Habari za wakati huu wapendwa wasomaji wetu na wafugaji,leo ningependa kuwaalika kujifunza kitu kidogo kuhusu kuku chotara na tofauti yake na kuku 100% asilia.
 Kuku chotara hutaga mayai mengi zaidi kulinganisha na kuku 100% asili.kuku chotara hutaga mayai 220-280 kwa mwaka kulingana na ubora wa chakula na mfumo mzima wa ufugaji.



Tetea wa chotara hula kiasi cha 6.8kg kwa muda wa miezi mitano na kuweza kufikia uzito wa 1.8kg kwa kipindi hicho.

Jogoo chotara huweza hula kiasi cha 6.8kg kwa muda wa miezi mitano na kuweza kufikia uzito wa 2.6 kwa muda huo.

Matetea chotara huanza kutaga ndani ya muda wa miezi mitano mpaka sita kutegemea na utunzaji na vyakula wanavyopewe.

Ili kuku hawa watage sana wanatakiwa kula angalau 122g kwa siku za chakula kizuri ili kuweza kutaga kwa muda mrefu.
Kuku hawa wataanza tabia ya kudonoana kama wasipopewa chakula kizuri na chenye virutubisho vya kutosha pamoja na madini.Kuku hawa hudonoana sana na wakati mwingine hupelekea vifo na vidonda


Wednesday 26 October 2016

Magonjwa ya kuku kwa ujumla yapo mengi sana na kuna baadhi ya magonjwa ambayo hayapo hapa nchini,ni vyema kujua dalili hizi za magonjwa mapema ili kuepusha hasara inayoweza kutokea kutokana na vifo ambavyo huchangiwa na magonjwa haya.
Dalili hizo kwa ujumla ni kama ifuatavyo
1.Kuku kupoteza hamu ya kula

2.Kuku kuzubaa na kukaa sehemu moja kwa muda mrefu
3.Kushuka kwa kiwango cha utagaji
4.Vifaranga kudumaa
5.Macho kua mekundu
6.Kujikunja shingo
7.Kutetemeka,kutoa maji maji puani,mdomoni na machoni
      8.Kutoa kinyesi chenye rangi ya kijani,au kinyesi kilicho changanyika na damu au cheupe.
9.  Kukohoa
10.  Kukonda sana

Endapo kuku wako ataonesha mojawapo ya dalili hizo basi mfugaji itamlazimu kutafta daktari wa mifugo au  kuku wapatiwe dawa.kujua madawa mbali mbali ya tazama post nyingine katika blog hii.Pia unaweza kufatilia mambo mbalimbali kuhusu kuku kupitia ukurasa wetu wa INSTAGRAM kwa jina la kukutajiri.

Kuku chotara/kienyeji hufungwa kwa matumizi ya kutaga mayai na pia kwa nyama.Mfugaji atachagua aina na mfumo wa chakula kutokana na yeye anafuga kuku hawa kwa matumizi gani.

Ili kuku wafugwe kwaajili ya mayai fuata ratiba hii ya chakula

Chick starter kwa muda wa miezi miwili(2)
Grower Mash kwa muda wa miezi miwili na nusu(2.5)
Layers mwezi mmoja na kuendelea.

Ili kuku wafugwe kwaajili ya nyama fuata ratiba hii ya chakula

Broiler starter-mwezi mmoja(1)
Grower Mash-Mwezi mmoja(1) 
Broiler Finisher-Mwezi mmoja(1)


Ili kuku wafugwe na kutaga mayai kwaajili kutotolesha fuata ratiba hii ya chakula

Chick Starter-miezi miwili(2)
Grower mash-miezi miwili na nusu(2.5)
Breeders mash-mwezi mmoja na kuendelea.hakikisha majogoo wanapunguzwa na kubaki na uwiano wa jogoo mmoja kwa matetea kumi(1:10)







Ratiba hii ni kwa ufugaji wa kibiashara lakin mfugaji anaweza kuwafuga kuku hawa kwa mfumo wa nusu huria yaani kuku akaachiwa ajitaftie chakula na kisha atapewa chakula na mfugaji.Pia kuku hawa huweza kufugwa huriaa yaani akaachwa kujitaftia chakula chake.



picha hapo juu ni vifaranga wa wiki moja baada ya kulishwa chick starter.

Sample Text

Powered by Blogger.

Pages

watembeleaji wa mtandao wetu

Popular Posts

kukutajiri on facebook

fuatilia makala zetu kupitia facebook kupitia ukurasa wetu wenye jina la hapo juu
//]]>