Friday, 11 March 2016

Magonjwa ya kuku kwa ujumla yapo mengi sana na kuna baadhi ya magonjwa ambayo hayapo hapa nchini,ni vyema kujua dalili hizi za magonjwa mapema ili kuepusha hasara inayoweza kutokea kutokana na vifo ambavyo huchangiwa na magonjwa haya.
 Dalili hizo kwa ujumla ni kama ifuatavyo

1.   
     Kuku kupoteza hamu ya kula
2.        Kuku kuzubaa na kukaa sehemu moja kwa muda mrefu
3.        Kushuka kwa kiwango cha utagaji

4.        Vifaranga kudumaa
5.        Macho kua mekundu
6.        Kujikunja shingo
7.        Kutetemeka,kutoa maji maji puani,mdomoni na machoni
8.        Kutoa kinyesi chenye rangi ya kijani,au kinyesi kilicho changanyika na damu au cheupe.
9.        Kukohoa
10.     Kukonda

Endapo kuku wako ataonesha mojawapo ya dalili hizo basi mfugaji itamlazimu kutafta daktari wa mifugo au  kuku wapatiwe dawa.kujua madawa mbali mbali ya tazama post nyingine katika blog hii.Pia unaweza kufatilia mambo mbalimbali kuhusu kuku kupitia ukurasa wetu wa INSTAGRAM kwa jina la kukutajiri.

Saturday, 27 February 2016

NENO LA USHAWISHI.......JE WEWE NI KIJANA NA UNAPENDA UFUGAJII???somaa hapaa

habari wasomaje na wafuatiliaji wa blog yetu,Leo ningependa kutoa neno la ushawishi kwa vijana wenzangu waliopo shuleni,vyuoni na mtaanii..je ni vipi unatumia muda wako baada ya masomo au kazi???umewahi kupata wazo la biashara??kama umewahi kupata wazo la biashara au la kukuingizia kipato ni kwanini hujaanza mpaka wakati huu???...MAWAZOO.......MAWAZOOO...Mawazo ni mazuri lakini yakifanyiwa kazi,mawazo yasipo fanyiwa kazi hakika kijana mwenzangu utabaki kuvusha tuu na kutamania maisha ya watu wengine.SIRI,siri ya mafanikio yoyote ni kufanya kazi,usiogope mtu mwenyewe mawazo makubwa,ila mheshimu sana mtu anaefanyia kazi mawazo yake.Hivyo siri ni moja,KUFANYA KAZI NA KUJITUMA KATIKA KILA JAMBO UFANYALO.


HII NI RATIBA YA CHANJO NA DAWA
1.     SIKU 1.
 Baada ya vifaranga kutotoreshwa wenye siku moja,vifranga wapewe glucose kwa muda wa masaa 2.Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa.baada ya hapo vifaranga wapewe vitamin mfano ni CHAMPRIX.Pia hii huchanganywa na maji.vifaranga wawe katika eneo lenye joto na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifanga wapewe OTC plus(kijiko kimoja cha chai katika lita 5 za maji safi,pia changanya vitamin.


2.       SIKU YA 7.
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDELI).chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kasha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye vitamin

mfano wa vifaranga wenye wiki moja(siku saba).Hawa wamepata chanjo ya newcastle na kama utakavyoona katika video hapa chini vifaranga wamechangamka.



3.     SIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD).chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewe vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu.baada ya hapo vifaranga wepewe vitamin.



4.     Siku ya 21.(wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle



5.     SIKU 28(mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD


6.     SIKU 35(mwezi 1 na wiki 1)
Kipindi hiki kuku wapewe vitamin ya kutosha.


7.     WIKI YA 6-8
KUKU wapatiwe kinga ya ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asie na utaalam kuwapa kuku,tafta mtaalum kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.
8.    WIKI YA 8
Kuku wapatiwe dawa ya minyoo na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle



Wednesday, 2 September 2015


Habari za wakati huu wafuatiliaje wa machapisho yetu.Leo tutatazamia njia kuu mbili za kutotoresha mayai ya kuku wa kienyeji,njia hizo ni kumuacha kuku kutotoa mwenyewe na kumuwekea mazingira.njia ya pili ni kwa kutumia mashine za kutotoreshea.


NJIA ASILIA
kwa kutumia njia hii kuku ataachwa kutaga,kuatamia,na kutotoa mwenywe.mfugaji aandae mabox au mfuko kisha aweke vitu vyenye kutunza joto kama mchanga au matambaa kisha mabox hayo yawekwe katika mabanda ya kuku sehemu tulivu na yenywe kivuli


kuku hugata mayai 10-14 kutegemeana na aina ya kuku.kuku huweza kutotoa mayai 8-14


NJIA YA KISASA
Baada ya kuandaa sehemu ya kuku kutagia,kusanya mayai kila siku na kuweka katika trei.Uwekaji wa mayai hayo,sehemu kubwa ya yai iwe juu na incha yake iangalie chini.Hii husaidia katika utotoleshaji kwenye mashine.mashine hutotoresha vizuri zaidi endapo mayai yatakua yalikusanywa katika kipindi kifupi kuanzia siku 1-6 na kuwekwa katika mashine (incubator)

 MASHINE YA KUTOTORESHEA VIFARANGA(INCUBATOR)
Hii ni mashine ambayo hufanya kazi ya kuatamia na kutotoa mayai.mashine ina uwezo wa kutoto mayai mengi,mashine ndogo huweza kutotoa mayai 25-50.mashine hii hutoa joto sawa na joto la tetea,inashauliwa kugeuza geuza mayai kwa siku angalau mara tatu katika mashine ili kupata mazao bora zaidi.


CHANGAMOTO YA MASHINE HII
Inahitaji utaalamu kuitumia
inahitaji muda mwingi kukaa nayo karibu
ni gharama kuiendesha.

Thursday, 27 August 2015


ni matumaini yangu wote mu wazima wa afya.katika chapisho hili tutaangalia njia za asilia za kutibu kuku kwa kutumia shubiri mwitu na majani ya mpapai.

SHUBIRI MWITU NA JINSI YA KUIANDAA
Tafta majani kadhaa ya shubiri mwitu kisha chana chana vipande vidogo vidogo kisha changanya na pumba na kuvianika.Mchanganyiko huo uanikwe juani.Baada ya kukauka vizuri twanga mchanganyiko huo ma kisha chekecha kupata unga.

majani ya shubiri mwitu

matumizi.
kuku walipata vidonda kutokana na magonjwa mbali mbali ,safisha vidonda vya kuku vizuri kisha pakaa unga huo katika vidonda hivyo.

pia hutumika kama chanjo.
kata kata vipande vidogo vidogo vya majani ya shubiri mwitu kisha changanya na maji na kuku wapewe maji hayo kwa wiki angalau mara tatu.maji yabadilishwe mara kwa mara kabla hayajaharibika.

MPAPAI NA NAMNA YA KUANDAA
mpapai husaidia kuku wanao harisha.
mti wa mpapai


maaandalizi
twanga majani ya mpapai kisha changanya na maji.majani mawili na maji lita mbili au moja na nusu.kuku wapewe maji hayo kwa siku nne lakini maji hayo yatengenezwe kila siku yasiachwe kiporo ili kutumika siku nyingine.


Ikitumika kama chanjo fanya kama ifuatavyo.

andaa kisamvu cha mpapai kisha changanya na pumba kg 2 mwsho weka na maji katika mchanganyiko huo kisha wape kuku lakini chakula hiki kiwekwe kulingana na idadi ya kuku kwa kua kisipo malizika mapema hualibika kirahisi.

kutibu minyoo

unga wa mbegu za mpapai husaidia sana kutibu minyoo katika kuku.

USIKOSE KUTEMBELEA BLOG YETU KUJUA MENGI KUHUSU KUKU.


Wednesday, 26 August 2015

Habari ndugu wasomaji wetu,leo tutachambua aina kadhaa za kuku wa kienyeji.Duniani kuna aina karibia 300 za kuku.katika toleo hili tutatazamia aina kubwa tatu za kuku wa kienyeji kibiashara.


1.KUCHI(rhode island)
kuku hawa wana sifa ya kutaga sana mayai na hawasumbuliwi sana na magonjwa pia hua na umbo kubwa sana.


2.CHOTARA(cross hybrid breeds)
Kuku hawa ni wakubwa na wanauzito mkubwa.kuku hawa ni wazuri kwa nyama lakini pia hutaga mayai mengi(10-13) kwa kuku mmoja.(hii si kwa siku moja ni katika mzunguko wa utagaji).kuku hawa ni wazuri kwa biashara huuzwa kuanzia 18,000/= mpaka 25000/= kutokana na mfugaji.




3.KUKU MALAWI 
Kuku hawa ni weusi na pia hua na maumbo makubwa sana,na wanasifa moja ya kutaga mayai mengi sana kuliko kuku wengine.



USIKOSE KUTEMBELEA BLOG YETU KUJUA ZAIDI KUHUSU KUKU WA KIENYEJI

shukrani za dhati.



habari za wakati huu ndugu wasomaji na wafuatiliaji wa blog yetu,leo tutaangalia namna ya kulea vifaranga.zifutazo ni hatua mbali mbali za maandalizi na mapokezi ya vifaranga.

1.MAANDALIZI YA BANDA
banda ni jambo la kwanza kwa mfugaji yoyote.banda la kuku huweza kujengwa kwa matofali,mbao,au hata miti na matope.
mfano wa banda la matofali lenye dirisha kubwa.
Banda la kuku linatakiwa liwe safi wakati wote.


1.Sifa za banda la kuku
lipitishe mwanga wa kutosha
lisiwe na nafasi ya wadudu hatari na hata wanyama kupita
liwe karibu na makazi ya mfugaji
sakafu yake isiwe na matobo tobo mengi(iwe imesakafiwa vizuri kwa njia tofauti)
banda liwe na ukubwa wa kutosha sawa na idadi ya vifaranga.(mita 2 kwa 3)
ndani ya banda kuwepo mabox madogo madogo kwaajili ya kuwekea vifaranga.mabox hutunza joto na chini ya mabox hayo au vitalu kuwepo na pumba za mahindi au mpunga ili kuongeza joto.
mfano wa box hilo katika picha.

2.Andaa vyombo
vyombo kwaajili ya maji na chakula.unaweza kununua vyombo ua ukatumia sahani  za kawaida za nyumbani.kwa maji weka mawe madogo madogo  masafi katika vyombo hivyo ili vifaranga wasitawanye sana maji au wao kuloana na maji hayo.
mfano wa vyombo katika picha


3.Andaa taa ya chemli au bulb
Taa hutumika kwaajili ya kuongeza joto katika box au kitalu cha vifaranga.taa huwekwa ndani ya box hilo.Kwa wafugaji wakubwa hutumia bulb katika mabanda yao.joto katika vifaranga liongezwe wakati wa usiku na mchana liwe la kawaida.



4.Fahamu ratiba na chanjo kwa vifaranga kama ifatavyo.

  • siku 1-5 --dawa ya kufunga vitovu-
  • siku 7 --NEWCASTLE
  • siku 8, 9,10,11--VITAMIN 
  • siku 14--Gomboro
  • Siku ya 15-20-VITAMIN
  • siku 21--gomboro Baada ya hapo endelea na vitamin hadi siku ya 27
  •  Siku ya 28-NEWCASTLE Kisha endelea na vitamin
  • wiki ya 5 chanjo ya ndui
  • wiki ya 6--Ampronium + ctc (siku tano)
  • wiki ya 7--Vitamin
  • wiki ya 8--dawa ya minyoo


ANGALIZO.EPUKA UCHAFU KATIKA BANDA ILI KUEPUSHA MAGONJWA KATIKA BANDA AMBAYO HUPELEKEA KUKU KUUMWA HIVYO KUTAFTIWA DAWA NYINGI ZAIDI NA KUPELEKEA KUONGEZEKA KWA GHARAMA ZA UFUGAJI.

5.CHAKULA

chakula cha kuku kiwe na mchanganyiko ufuatao.

  • nafaka(mahindi,uwele,mtama,ulezi nk)-------kg 40
  • pumba za nafaka_----------------------kg 27
  • chumvi ya jikoni--------------kg 0.5
  • virutubisho----------------------kg 0.05
  • unga wa chokaa na mifupa-----kg 2.25
  • mashudu ya alizeti ufuta au karanga --kg 20
  • dagaa na mabaki ya samaki---kg 10


6.ANDAA KUMBU KUMBU MUHIMU IWE NA;


  • tarehe ya kutotoresha
  • idadi ya vifaranga
  • kiasi cha chakula
  • vifo
  • vifaranga vilivyo uzwa
  • tarehe ya siku ya kurekodi
  • matibabu
  • ugonjwa
  • mfano wa ratiba hiyo



ENDELEA KUFATILIA BLOG HII KUJUA ZAID KUHUSU KUKU WA KIENYEJI
Ahsanteni.




Sample Text

Powered by Blogger.

Pages

watembeleaji wa mtandao wetu

Popular Posts

kukutajiri on facebook

fuatilia makala zetu kupitia facebook kupitia ukurasa wetu wenye jina la hapo juu
//]]>