Wednesday, 31 May 2017

SEHEMU YA KWANZA
Tumerahisisha zaidi maelezo na kuifanya iakisi mazingira harisi ya mfugaji wa kitanzania
Hydroponic ni nini?
Ni mbinu ya kukuza mimea kwa kutumia mchanganyiko wa virutubisho vya madini katika maji bila kutumia udongo. Mchakato huu huchukua siku 6 hadi tisa kukamilika.
Kilo moja ya mbegu huzalisha wastani wa kilo 6 hadi kumi za majani na mizizi.



Faida za Teknolojia hii
i. Malisho huzalishwa ndani ya muda mfupi katika eneo dogo.mfano eneo la 4X3 mita huweza kutoa malisho sawa na ekari 2.
ii. Chakula hiki hulika chote kwa mifugo. Wanakula najani yote pamoja na mizizi. Hakuna upotevu wa chakula.
iii. Mahitaji ya maji ni madogo na maji yanaweza kutumika tena na tena.
iv. Gharama za uendeshaji wake ni mdogo; hakuna kuandaa ardhi, palizi na gharama za uvunaji.
v. Uwezekano mdogo sana wa wadudu ama magonjwa kushambulia.
Faida katika ulishaji
i. Chakula hiki ni laini hivyo mmengényo wake katika mifugo ni mkubwa hivyo sehemu kubwa hutumika katika mwili wa mifugo na uzalishaji.
ii. Mazao ya mifugo uboreka zaidi na kuendana na mahtaji ya soko. Mfano:
mayai ya kuku huwa na kiini cha njano zaidi wanapokula majani.
Maziwa huwa na uwiano mzuri wa Omega 3 na Omega 6 amino acid ambazo hujenga afya imara ya mlaji.
iii. Hupunguza gharama za chakula na hivyo kuongeza faida.
iv. Virutubisho vingi hasa vitamin ambazo huchangia afya ya mifugo kuimalika.
v. Kinapolishwa kwa mchanganyiko na vyakula vingine kwa uwiano tutakaoutoa hapo mbele, uzalishaji na ukuaji wa mifugo huwa mzuri zaidi.




Vifaa mihimu
Sehemu/chumba cha kukuzia.
Nguzo na fito za kutengeneza chanja kwa ajili ya kupanga trei.









 Trei za plastiki/aluminiamu.









 Dawa yenye Chlorine (kama Waterguard) ama JIK kuua vijidudu katika maji na mbegu.
Virutubisho (nutrients): wengine hutumia buster za mazao (hakikisha haina madhara kwa mifugo).









 Pump (sprayer) kunyunyiza maji.
Mbegu.


Mbegu zinazoweza kutumika
 Shayiri, mahindi, ngano, mtama na nafaka nyingine nyingi.



SEHEMU YA PILI


UZALISHAJI WA MALISHO KWA TEKNOLOJIA YA HYDROPONIC
SEHEMU YA PILI

HATUA KWA HATUA KATIKA KUZALISHA HYDROPONIC
Kwa kufata hata hizi unaweza kuzalisha malisho yako mwenyewe nyumbani.
1. Chagua mbegu ambazo hazijaanza kuchipua, na hazina kemikali ama dawa ya aina yoyote.
2. Loweka mbegu katika mchanganyiko wa maji na Chlorine kwa masaa mawili kuepusha kuvu/uvundo ama vimelea vya magonjwa kumea na kukua.
3. Zitoe mbegu kwenye maji, zioshe kisha ziloweke kwenye maji safi kwa masaa 24 kuwezesha mbegu kufyonza maji vema.
4. Katika kupanda mbegu, pima kilo mbili za mbegu kwa kila trei yenye urefu wa Cm 80 kwa upana wa  Cm 40.
5. Sambaza mbegu kwenye trei kwa usawa, (zisizidi Cm 3 kimo) ili kuwe na nafasi ya kutosha kwa kila mbegu kuchipua (kuota).
6. Hakikisha trei zina matundu kwenye kitako (chini) ambayo yamesambaa kwa usawa kuwezesha maji ya ziada kutoka.
7. Hamishia trei kwenye chanja ulizotengeneza. Mbegu zitaanza kuota katika hatua hii. Fanya hii ni siku ya kwanza.
8. Nyunyizia maji (kwa pampu) toka siku ya kwanza hadi ya sita, kwa mara nne katika kila masaa 24.

ZINGATIA.
Mbegu zenye dawa au sumu yoyote ni hatari kwa wanyama. zinaweza kuwadhoofisha ama kuwaua. hakikisha hautumii mbegu zenye dawa.

Jinsi ya kulisha

Kuku: kwa kuku 100 wanaotaga (layer) wape kilo 8  za hydroponics na waongezee kilo 4 za chakula cha layer (layer mash) kwa siku.

Nguruwe: katika unenepeshaji wape kilo 2 za hydroponics na 1.5 za chakula kikavu (nafaka) kwa nguruwe mmoja kwa siku.

Ngómbe, mbuzi: wanaweza kutegemea majani haya tu na kuwa na uzalishaji mzuri bila nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka. Kama uzalishaji wa maziwa ni mkubwa sana (zaidi ya lita 12 kwa siku) ni vema kuwaongezea nafaka.

Sungura: wanaweza kutegemea majani haya tu lakini ni vema kuwapa nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka (angalau kwa uwiano wa 50%).

MAJIBU YA MASWALI.
TREI: wengi mliuliza kuhusu upatikanaji wa trei. Trei tumeagiza na bei ni shilingi elfu saba moja. Weka oda mapema katika namba chini.
NUTRIENTS: wengine mliuliza kuhusu mbolea. mbelea ni adimu na bei kubwa. kwa uchunguzi tulioufanya BOOSTER ya mimea hasa yenye NPK inaweza kutumika kama mbadala wa nutrients. kama tulivyoeleza kwenye sehemu ya kwanza. booster ichanganywe na maji kabla ya kumwagilia.
matumizi ya nyungo. unaweza kutumia ungo kupanda hyadroponi. ila ni ghali kwa sababu ungo huoza haraka sababu ya unyevunyevu wakati wote. ivyo ni muhimu kununua trei zinazodumu siku zote.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na kuweka order ya trei : 0755639835


Monday, 27 February 2017

Habari wapenzi wasomaji wetu,Leo napenda kuwaletea biashara ya vifaranga wa kuku chotara.Vifaranga wa mwezi mmoja wakiwa na chanjo kama
1.NEWCASTLE
2.GUMBORO
3. NDUI,

Pia wanunuzi wa vifaranga watapewa semina fupi kabla ya kupewa vifaranga.



Picha ya hapa chini ni baadhi ya vifaranga chotara wakina na mwezi mmoja.


Picha ya hapa chini ni vifaranga wa siku moja




Vifaranga hapa chini ni vifaranga wa wiki moja


 Wafugaji kutoka KUKUTAJIRI katika kazi ya ukusanyaji mayai kwaajili ya kwenda kutotolesha,je unajua sifa ya mayai bora kwaajili ya kutotolesha?endelea kufuatilia mtandao wetu utajifunza sifa hizo.

hapa chini ni kuku walezi kwaajili ya utagaji mayai ili yakatotoleshwe 

hapa chini ni aina ya jogoo kutoka kukutajiri.


kuku wazazi wakipewa chakula na wafugaji kutoka kukutajiri

bei ya vifaranga ni;
VIFANGA WA MWEZI NI TSH 4000/=
VIFARANGA WA SIKU NI TSH 2000/=
wasiliana nasi kwa namba 0719342444 au 0718616834

Tuesday, 1 November 2016

Habari za wakati huu wapenzi wasomaji wetu,Leo ningependa kutoa mawazo yangu kuhusu suala la kilimo nchini.
Tanzania ni nchi maskini,uchumi wa nchi hii unategemea zaidi kilimo.Kilimo huchangia asilimia 50 ya pato la ndani la nchi hii.Kumekua na jitihada mbalimbali za kuendeleza sekta hii ya kilimo nchini ikiwemo sera iliyo sikika sana ya "KILIMO KWANZA" .Jitihadi hizi zimeweza kufanikiwa kwa kiasi fulani ila kwa kiasi fulani bado uzalishaji wa malighafi nchi bado ni mdogo.
Baada ya kuhudhuria semina mbalimbali nilishangazwa kusikia hadi kuku tunaagiza kutoka nchi za jirani kama Malawi na Kenya.Ni aibu kubwa kwa taifa kama hili lenye ardhi kubwa na rasilimali watu.


VIFARANGA ZAIDI YA 5000 WALIOKAMATWA AIRPORT WAKIINGIZWA NCHINI KWA NJIA HARAMU

Nadhani ni wakati serikali ijaribu kutumia vijana wahitimu katika vyuo mbali mbali katika kuendeleza suala la kilimo nchini. Sera ya  KILIMO KWANZA ilikua na nia nzuri lakini imeonekana kama ilikua na nguvu ya soda,na pia ingelenga vijana moja moja ili kupunguza tatizo la ajira.
Pia vijana waelimishwe kuhusu kilimo,ufugaji na uvuvi ili waweze kujiajiri katika sekta hiyo.Nadhani iwepo sera kwaajili ya kuwahimiza vijana kuhusu kilimo na pia wapewe elimu na mikopo ili waweze kuingia katika uzalishaji malighafi kwa sababu tanzania ya viwanda inakuja hivyo vijana tuwe na Tanzania ya KILIMO ili tuweze kwenda sawa na kasi ya ukuaji wa teknolojia katika viwanda kwani viwanda vitahitaji malighafi hivyo si vyema kuagiza malighafi hizo nje ya nchini wakati nchi ina nguvu kazi na ardhi ya kutosha. Vijana turudi mashambani Tanzania ya tuijenge.

"VIJANA NA TANZANIA YA KILIMO"

KILIMO CHA CHIKICHI NA UTAJIRI KWA MKULIMA

KILIMO CHA UFUTA

UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI NA MASOKO YAKE

Thursday, 27 October 2016

Habari za wakati huu wapendwa wasomaji wetu na wafugaji,leo ningependa kuwaalika kujifunza kitu kidogo kuhusu kuku chotara na tofauti yake na kuku 100% asilia.
 Kuku chotara hutaga mayai mengi zaidi kulinganisha na kuku 100% asili.kuku chotara hutaga mayai 220-280 kwa mwaka kulingana na ubora wa chakula na mfumo mzima wa ufugaji.



Tetea wa chotara hula kiasi cha 6.8kg kwa muda wa miezi mitano na kuweza kufikia uzito wa 1.8kg kwa kipindi hicho.

Jogoo chotara huweza hula kiasi cha 6.8kg kwa muda wa miezi mitano na kuweza kufikia uzito wa 2.6 kwa muda huo.

Matetea chotara huanza kutaga ndani ya muda wa miezi mitano mpaka sita kutegemea na utunzaji na vyakula wanavyopewe.

Ili kuku hawa watage sana wanatakiwa kula angalau 122g kwa siku za chakula kizuri ili kuweza kutaga kwa muda mrefu.
Kuku hawa wataanza tabia ya kudonoana kama wasipopewa chakula kizuri na chenye virutubisho vya kutosha pamoja na madini.Kuku hawa hudonoana sana na wakati mwingine hupelekea vifo na vidonda


Wednesday, 26 October 2016

Magonjwa ya kuku kwa ujumla yapo mengi sana na kuna baadhi ya magonjwa ambayo hayapo hapa nchini,ni vyema kujua dalili hizi za magonjwa mapema ili kuepusha hasara inayoweza kutokea kutokana na vifo ambavyo huchangiwa na magonjwa haya.
Dalili hizo kwa ujumla ni kama ifuatavyo
1.Kuku kupoteza hamu ya kula

2.Kuku kuzubaa na kukaa sehemu moja kwa muda mrefu
3.Kushuka kwa kiwango cha utagaji
4.Vifaranga kudumaa
5.Macho kua mekundu
6.Kujikunja shingo
7.Kutetemeka,kutoa maji maji puani,mdomoni na machoni
      8.Kutoa kinyesi chenye rangi ya kijani,au kinyesi kilicho changanyika na damu au cheupe.
9.  Kukohoa
10.  Kukonda sana

Endapo kuku wako ataonesha mojawapo ya dalili hizo basi mfugaji itamlazimu kutafta daktari wa mifugo au  kuku wapatiwe dawa.kujua madawa mbali mbali ya tazama post nyingine katika blog hii.Pia unaweza kufatilia mambo mbalimbali kuhusu kuku kupitia ukurasa wetu wa INSTAGRAM kwa jina la kukutajiri.

Kuku chotara/kienyeji hufungwa kwa matumizi ya kutaga mayai na pia kwa nyama.Mfugaji atachagua aina na mfumo wa chakula kutokana na yeye anafuga kuku hawa kwa matumizi gani.

Ili kuku wafugwe kwaajili ya mayai fuata ratiba hii ya chakula

Chick starter kwa muda wa miezi miwili(2)
Grower Mash kwa muda wa miezi miwili na nusu(2.5)
Layers mwezi mmoja na kuendelea.

Ili kuku wafugwe kwaajili ya nyama fuata ratiba hii ya chakula

Broiler starter-mwezi mmoja(1)
Grower Mash-Mwezi mmoja(1) 
Broiler Finisher-Mwezi mmoja(1)


Ili kuku wafugwe na kutaga mayai kwaajili kutotolesha fuata ratiba hii ya chakula

Chick Starter-miezi miwili(2)
Grower mash-miezi miwili na nusu(2.5)
Breeders mash-mwezi mmoja na kuendelea.hakikisha majogoo wanapunguzwa na kubaki na uwiano wa jogoo mmoja kwa matetea kumi(1:10)







Ratiba hii ni kwa ufugaji wa kibiashara lakin mfugaji anaweza kuwafuga kuku hawa kwa mfumo wa nusu huria yaani kuku akaachiwa ajitaftie chakula na kisha atapewa chakula na mfugaji.Pia kuku hawa huweza kufugwa huriaa yaani akaachwa kujitaftia chakula chake.



picha hapo juu ni vifaranga wa wiki moja baada ya kulishwa chick starter.

Friday, 11 March 2016

Magonjwa ya kuku kwa ujumla yapo mengi sana na kuna baadhi ya magonjwa ambayo hayapo hapa nchini,ni vyema kujua dalili hizi za magonjwa mapema ili kuepusha hasara inayoweza kutokea kutokana na vifo ambavyo huchangiwa na magonjwa haya.
 Dalili hizo kwa ujumla ni kama ifuatavyo

1.   
     Kuku kupoteza hamu ya kula
2.        Kuku kuzubaa na kukaa sehemu moja kwa muda mrefu
3.        Kushuka kwa kiwango cha utagaji

4.        Vifaranga kudumaa
5.        Macho kua mekundu
6.        Kujikunja shingo
7.        Kutetemeka,kutoa maji maji puani,mdomoni na machoni
8.        Kutoa kinyesi chenye rangi ya kijani,au kinyesi kilicho changanyika na damu au cheupe.
9.        Kukohoa
10.     Kukonda

Endapo kuku wako ataonesha mojawapo ya dalili hizo basi mfugaji itamlazimu kutafta daktari wa mifugo au  kuku wapatiwe dawa.kujua madawa mbali mbali ya tazama post nyingine katika blog hii.Pia unaweza kufatilia mambo mbalimbali kuhusu kuku kupitia ukurasa wetu wa INSTAGRAM kwa jina la kukutajiri.

Sample Text

Powered by Blogger.

Pages

watembeleaji wa mtandao wetu

Popular Posts

kukutajiri on facebook

fuatilia makala zetu kupitia facebook kupitia ukurasa wetu wenye jina la hapo juu
//]]>