Thursday, 20 August 2015


habari za wakati huu wapendwa wafugaji na wasio wafugaji,wasomi wa machapisho yetu kwa ujumla.katika toleo hili tunachambua magonjwa mbalimbali ya kuku.magonjwa ya kuku husabibishwa na vitu mbali mbali ikiwemo virusi,minyoo,bakteria,uchafu,wadudu na hata upungufu wa virutubisho katika vyakula vya kuku hawa.magonjwa ambayo husababishwa na virusi hua ni vigumu sana kutibika hivyo mfugaji hushauliwa kuwapa chanjo ya magonjwa hayo.mfano ni mdondo(new castle disease).ugonjwa huu ni hatari sana kwa kua humaliza kuku wengi kwa wakati mmoja.wengine huita huu ugonjwa kideri.
   Mdondo(new castle disease).
kama binadamu aogopavyo ugonjwa wa UKIMWI,basi wafugaji wengi huogopa sana ugonjwa wa mdondo,pia huitwa kideli(newcastle disease).huu ni ugonjwa HATARI unaosababishwa na virusi pia ni ugonjwa huu hauna tiba.Hivyo mfugaji anatakiwa kuwapa chanjo mapema kabla ugonjwa haujafika eneo hilo.dalili za mdondo ni kama.
1.kuku kukohoa au kuhema kwa tabu
2.manyoya ya kuku huvurugika na kua katika hali isiyo ya kawaida.
3.kuku huarisha kinyesi cha kijani
3.kupoteza hamu ya kula na mabawa kupoza
4.kizunguzungu na kuanguka chali
5.kupoteza fahamu

ugonjwa huu hupelekea kuku wengi kufa kufikia hadi asilimia 50 hadi 100 kama usipo dhibitiwa mapema.
Namna ya ugonjwa unavyosambaa
1.virusi hawa huweza kusambaa kwa njia ya hewa au upepo husafirisha virusi hawa.
2.kinyesi cha kuku mwenye mdondo kikikanyagwa na mtu,baiskeli au wanyama wengine na kusafirishwa kwenye banda la kuku,ugonjwa huu huweza pia kusambaa.
3.kuku alie kufa kwa mdondo asipo zikwa vizuri au kuchomwa moto,kuku mzima akila mabaki hayo,kuku hao watakua katika hatari ya kupata mdondo.
JINSI YA KUPAMBANA NA MDONDO
Kama ilivyo elezwa hapo juu,gonjwa hili halina tiba.lakini kuku wakipewa chanjo kwa wakati hua katika usalama.kuna chanjo kama;
1.LASOTA
chanjo hii ni ya vidonge,kidonge kimoja huchanganjwa na maji safi.chanjo hii tolewa baada ya siku tatu kisha rudi baada ya wiki tatu  na rudia kila baada ya majuma manne au kutokana na uonavyo.kabla ya kuku kupewa dawa hii yapaswa wasipewe maji kwa masaa kadhaa kwa siku hio na muda wa kupewa maji basi wapewe sehemu yenye kivuli.
chanjo hii hupatikana katika maduka mbali mbali ya mifugo.
2.Chanjo ya Thermostable 1-2,dawa hii inahuwezo mkubwa wa kustahimili joto,watu wasio na majokofu basi tumia dawa hii ila hifadhi sehem kavu na isio na joto.dawa  hii huweza kukaa wiki mbili baada ya kufunguliwa kwa Mara ya kwanza.
EPUKA YAFUATAYO
kununua kuku katika minada na kuleta bandani
kuruhusu kila mtu kuingia katika banda la kuku
kuacha mabaki ya kuku walikufa ovyo katika mazingira ya kuku
pia,endapo kuku wengi walikufa katika banda hilo basi ni vyema usilete kuku wengine katika banda hilo angalau kwa ,mwezi au zaid.
Tenganisha kuku wenye dalili za ugonjwa na kuku wengine.
ZINGATIA USAFI WA BANDA NA VYOMBO VYA KUKU WAKO.

usikose kutembelea blog hii kwa taarifa nyingine zaidi kuhusu ufugaji wa kuku



Related Posts:

  • NENO LA USHAWISHINENO LA USHAWISHI.......JE WEWE NI KIJANA NA UNAPENDA UFUGAJII???somaa hapaa habari wasomaje na wafuatiliaji wa blog yetu,Leo ningependa kutoa neno la ushawishi kwa vijana wenzangu waliopo shuleni,vyuoni na mtaanii..je ni vi… Read More
  • NJIA ASILIA ZA KUTIBU KUKU ni matumaini yangu wote mu wazima wa afya.katika chapisho hili tutaangalia njia za asilia za kutibu kuku kwa kutumia shubiri mwitu na majani ya mpapai. SHUBIRI MWITU NA JINSI YA KUIANDAA Tafta majani kadhaa ya shubiri mwitu… Read More
  • KUTOTORESHA VIFARANGA Habari za wakati huu wafuatiliaje wa machapisho yetu.Leo tutatazamia njia kuu mbili za kutotoresha mayai ya kuku wa kienyeji,njia hizo ni kumuacha kuku kutotoa mwenyewe na kumuwekea mazingira.njia ya pili ni kwa kutumia mash… Read More
  • JE WAJUA RATIBA YA CHANYO YA KUKU ASILIA/BROILERS??soma hapaaa HII NI RATIBA YA CHANJO NA DAWA 1.     SIKU 1.  Baada ya vifaranga kutotoreshwa wenye siku moja,vifranga wapewe glucose kwa muda wa masaa 2.Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa… Read More
  • DALILI ZA JUMLA ZA KUKU Magonjwa ya kuku kwa ujumla yapo mengi sana na kuna baadhi ya magonjwa ambayo hayapo hapa nchini,ni vyema kujua dalili hizi za magonjwa mapema ili kuepusha hasara inayoweza kutokea kutokana na vifo ambavyo huchangiwa na mago… Read More

0 comments:

Post a Comment

watembeleaji

A visitor from Dar es salaam viewed 'NJIA ASILIA ZA KUTIBU KUKU ~ fahamu uleaji wa kuku' 11 hrs 49 mins ago
A visitor from Terre haute viewed '2017 ~ fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 2 days 6 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed '2017 ~ fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 2 days 6 hrs ago
A visitor from Yekaterinburg viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 2 days 14 hrs ago
A visitor from Mwanza viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 3 days 6 hrs ago
A visitor from Rostov-on-don viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 3 days 11 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 4 days 11 hrs ago
A visitor from Gauteng viewed 'JE WAJUA,JINSI YA KULEA VIFARANGA?..soma hapa ~ fa' 5 days 6 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 7 days 6 hrs ago
A visitor from Nuremberg viewed '2015 ~ fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 7 days 21 hrs ago

Sample Text

Powered by Blogger.

Pages

watembeleaji wa mtandao wetu

A visitor from Dar es salaam viewed 'NJIA ASILIA ZA KUTIBU KUKU ~ fahamu uleaji wa kuku' 11 hrs 49 mins ago
A visitor from Terre haute viewed '2017 ~ fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 2 days 6 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed '2017 ~ fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 2 days 6 hrs ago
A visitor from Yekaterinburg viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 2 days 14 hrs ago
A visitor from Mwanza viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 3 days 6 hrs ago
A visitor from Rostov-on-don viewed 'RATIBA YA CHAKULA KWA KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA ' 3 days 11 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 4 days 11 hrs ago
A visitor from Gauteng viewed 'JE WAJUA,JINSI YA KULEA VIFARANGA?..soma hapa ~ fa' 5 days 6 hrs ago
A visitor from Dar es salaam viewed 'fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 7 days 6 hrs ago
A visitor from Nuremberg viewed '2015 ~ fahamu uleaji wa kuku wa kienyeji' 7 days 21 hrs ago

Popular Posts

kukutajiri on facebook

fuatilia makala zetu kupitia facebook kupitia ukurasa wetu wenye jina la hapo juu
//]]>